CHAMA CHA MAZINGIRA NA UFUGAJI TIJA TANZANIA (CHAMAUTA)
“Tunza Mazingira, Fuga kwa Tija kwa Maendeleo ya Taifa”
MPYA
Taarifa ya Usajili kidijitali
MAELEKEZO YA NAMNA YA KUSAJILI WANACHAMA WAPYA MIKOANI:
Zoezi la Kusajili Wanachama wapya Kidigital huko Mikoani ni endelevu. Utaratibu ni kama ufuatao:-
1. Mwananchi aliye tayari kujiunga na CHAMAUTA anatakiwa kujaza Fomu ya kuomba kujiunga.
2. Kila Fomu ibandikwe Picha ya muombaji.
3. Fomu irudishwe makao makuu kwa njia ya mtandao (MAKAO MAKUU).
4. Fomu zikisha hakikiwa. Na malipo ya Kiingilio na Ada ya Mwanachama TShs. 10,000/- (elfu kumi tu) ikishawekwa kwenye namba Account ya CHAMAUTA, Benki ya CRDB.
5. KADI yake itatumwa mara moja kupitia Uongozi wa eneo husika (Wilaya au Mkoa). Hiyo ni njia moja. PILI Mahali wanapopatikana kwa wingi kwa wakati mmoja Wanachama wapya *300 - 500+.* Tutatuma Kikosi kazi cha Viongozi na Watalaam kwenda na vifaa kutoa na kukabidhi KADI papo hapo.
Pakua fomu hapa chini ya kujiunga CHAMAUTA kwa mtu binafsi.
Pakua fomu chini ya kujiunga CHAMAUTA kwa Kikundi/Taasisi/Kampuni.
KUHUSU SISI
Chama cha Mazingira na Ufugaji Tija Tanzania (CHAMAUTA) ni chama kilichoundwa na wadau mbalimbali wa utunzaji wa mazingira pamoja na ufugaji wenye tija hapa nchini. Wadau hao ni wale wanaofuga mifugo mbalimbali kama vile ng’ombe, kondoo, mbuzi, nguruwe, Samaki, Bata, Sungura n.k. Msukumo wa kuanzisha chama hiki unatokana na hitaji la kuongeza tija katika ufugaji na kutunza na kuendeleza mazingira ambayo mifugo hiyo hutegemea.
Chama kimesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya usajili wa vyama vya Kijamii (The societies Act (CAP 337 R.E 2002) na Kupewa namba ya usajili S.A 23417 Ya tarehe 3 augost, 2023.
JEREMIAH JOHN WAMBURA
Mwenyekiti Taifa Chama Cha Mazingira na Ufugaji Tija Tanzania
Kazi ya Taasisi
Kuunganisha Nguvu za wadau wote wa utunzaji wa mazigira na wafugaji wote Tanzania, ili kulinda na kutetea haki na maslahi yao kuimarisha na kutafuta Masoko ya mifugo na kuwajengea uwezo kibiashara na kiuchumi ili kuweza kujiendeleza. Kuhakikisha wafugaji wanapata maeneo bora ya malisho yenye kuendana na dhima nzima ya ufugaji wenye Tija na utunzaji wa mazingira
Taasisi inaamini katika Mambo yafuatayo
➢ Uwazi
➢ Heshima
➢ Uwajibikaji
➢ Uzalendo
➢ Kujitolea
➢ Umoja
➢ Kuzigatia Matokeo Chanya
➢ Kazi kwa pamoja
➢ Mazingira Rafiki
➢ Ubora